Alexis Sanchez wa Man Utd ahukumiwa jela miezi 16....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.
Alexis Sanchez
Lakini amelipa faini ya pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.
Hukumu hiyo imetolewa jana ,Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela.

Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search