Ripoti wizi mali za waislam mezani kwa rais Magufuli......soma habari kamili na matukio360....#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema taarifa ya tume iliyokuwa ikichunguza mali za waislam nchini imefikishwa kwa rais John Magufuli.


Mufti wa Tanzania, sheikh Abubakar Zuberi

Akizungumza katika mahojiano maalum na matukio360  hivi karibuni jijini Dar es salaam, mufti Zuberi amesema ripoti hiyo imekamilika na wameifikisha kwa rais ili hatua zaidi zichukuliwe.


"Tume ilikamilisha taarifa za mali za waislam zilizoibwa, zilizopotea na taarifa zake zipo na zimekusanywa vizuri. Na tayari  tumeshazifikisha kwa rais Magufuli zipo mezani kwake kwa hatua zaidi, "amesema.


Amesema taarifa hiyo ilipelekwa kwa rais muda mrefu na kinachosubiliwa ni utekelezaji na majibu ya rais.

Kuhusu utendaji wa Bakwata amesema shughuli za kila siku za baraza hilo unakwenda vizuri kutoka na kuwepo kwa  hali ya utulivu na kwamba awali kulikuwa hujuma za chini kwa chini.

"Kwa kweli awali Bakwata kulikuwa na fitina za ndani kwa ndani na nje pia ndiyo maana hakukuwa na maendeleo kwa zaidi ya miaka 50. Lakini sasa utulivu umepatikana na utendaji wa kila siku unakwenda vizuri," amesena


Amewataka waislam wajitambue, wabadilike na kuacha mazoea na kutengeneza dhambi kwa kuweka vigenge kwa kufanya fitina.


Akizungumzia hatua ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulitaka Baraza Kuu la Waislam (Bakwata) mkoani Dar es salaam kumuorodheshea  maeneo ya waislam yaliyoporwa ili ashughulike nayo sheikh Zuberi amempongeza.


"Ni jambo zuri sana na tutalifanyia kazi ,na kazi yenyewe imeshakwisha tutakachokifanya tutatoa 'document ' ya mkoa wa Dar es Salaam, "amesema.


Amesema taarifa za tume iliyokuwa ikikusanya taarifa za kupotea na kuibiwa kwa mali za waislam ilianzia Dar es Salaam hivyo taarifa hizo zipo.


"Zingine ambazo zitakuwa zimejitokeza tutamuambataniashia kama kiambatanisho tutampa Makonda, "amesema.

Hivi karibuni akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa makao makuu ya Bakwata na shule ya sekondari Kinondoni, utakaogharimu bilioni 4.5 pamoja  na  mambo mengine Makonda aliomba orodha hiyo na aombewe kwa M/Mungu ili aweze kuwasaidia watu na kupata haki zao.

"Ninaomba mniletee orodha  ya maeneo ya Bakwata ya Dar es Salaam yaliyoporwa nataka kushughulika nayo ambayo wajanja wajanja wameyaingilia, "alisema.


Aliwahakikishia maeneo hayo yatapatikana ili waislamu wafanye mambo yao ya maendeleo.


Pia Makonda aliwataka waumini wa madhehebu yote nchini kuwathamini viongozi wao bila kusubiri kuombwa msaada.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search