Wanandoa wakamatwa wizi mtoto mchanga hospitalini...soma habari kamili na matukio360.....#share


Na mwandishi wetu, Mbeya.


WANANDOA, Peter Chiluba na mkewe Happy Charles wanashikiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mtoto wa siku moja aliyeibwa Februari mosi, 2018 katika wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Mbeya


Siku hiyo majira ya saa 9.00 alfajiri , mwanamke
huyo alijifanya muuguzi na kuingia katika wodi ya wazazi na
kumchukua mtoto wa Sarah Mwasanga (40) aliyejifungua kwa upasuaji kwa madai ya kwenda kumpatia chanjo,

Mama wa Mtoto Sarah Mwasanga (40) akiwa katika hospitali ya
wazazi Meta mara baada ya kupatikana kwa mtoto huyo katika kata ya uyole, jana .

Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa, Yahaya Msuya amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao wakazi wa kata ya uyole kulitokana na ushirikiano baina ya wananchi, uongozi wa hospitali na jeshi la polisi.


Amesema uchunguzi unaonyesha kabla ya wanandoa hao kufika
katika hospitali ya mkoa walifika katika hosptali ya wazazi Meta
ambapo jitihada zao zilishindikana.

"Baada ya muda mwanamke huyo alikodi pikipiki hadi hospitali ya mkoa akiwa amebeba kitu mfano wa mtoto na alipohojiwa na walinzi alieleza kuwa ana mtoto mgonjwa kaandikiwa sindano za saa na hivyo kuruhusiwa "alisema.


Msuya amesema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na yuko
katika uangalizi wa madaktari kutoka na mazingira waliyomkuta baada ya kuibwa,.

Mama wa mtoto huyo, Sarah Mwasanga(40) amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa alitokwa na damu nyingi na kuishiwa nguvu mara baada ya kuibiwa mtoto wake.

"Siamini kilichotokea, nilitambua mwanagu amechukuliwa kimazingira na mwanamke aliyefika katika wodi ya wazazi (juzi) saa tisa za usiku akiwa kama muuguzi kwa kweli yote namwachia Mungu,"amesema

Baba wa mtoto, Michael Mwasanga amesema Januari 30, 2018 alimfikisha mkewe kwa ajili ya kujifungua na walipokelewa na wauguzi katika wodi ya wazazi na kwa bahati nzuri Mungu alisaidia akajifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanawashikilia wanandoa hao kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.

Amesema bado wanaendelea na taratibu za kisheria za kuwahoji na watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika na kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa .

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search