Akamatwa na dawa za kulevya uwanja wa ndege...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


JESHI la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege jijini Dar es Salaam, linamshikilia raia wa Nigeria, Christian Ugbechi(26) akiwa na pipí 59 zenye zaidi ya gram 800 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.



Akizungumza na matukio360 kamanda wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema Januari 29 majira ya 8:15 mchana eneo la ukaguzi abiria wa nje uwanjani hapo walimtilia shaka abiria huyo.


 "Mnigeria huyo anaishi na kufanya kazi nchini ufaransa alikuwa akisafiri na ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia kuelekea Ufaransa kupitia Adis Ababa Ethiopia,"amesema.


Amesema pipi 56 amezificha ndani ya boksi alilokuwa amebeba mgongoni huku tatu akiwa amemeza tumboni.


"Bado yupo chini ya uangalizi maalum wa Polisi kuhakikisha anazitoa pipi zote alizomeza tumboni,"amesema.


Amefafanua kuwa jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu mwenye nia ovu kupitia viwanja vya ndege kusafirisha dawa za kulevya kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search