Sirro amtahadharisha kamishna mpya wa polisi Zanzibar....soma habari kamili na matukio360....#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini(IGP),Simon Sirro amemtaka Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Hassan Haji kuangalia na kuvishughulikia viashiria vya ugaidi na ucheleweshaji wa upelelezi Zanzibar.


Pia kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu, kupambana na rushwa,dawa za kulevya na usalama barabarani.

Kamishna mpya wa polisi Zanzibar akila kiapo leo jijini Dar es salaam

Sirro ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kumuapisha Kamishna wa Zanzibar, Haji baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli.

Amesema jeshi la Polisi wanakazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utulivu na amani.

Amesema suala la ucheleweshwaji wa kesi si la Polisi pekee bali zipo kesi zingine hupelelezwa na vitengo vingine hivyo watahakikisha wanaimba wimbo mmoja na kwamba wanawashughulikia na kuwafukuza askari wenye udhaifu.

"Idara nyingine ambazo IGP hana mamlaka nazo ni kukaa nazo pamoja na kuwekeana mkakati wa pamoja kuhakikisha wanawatendea haki watanzania.

"Changamoto tunazo kubwa na rais amekuwa anazungumza mara nyingi changamoto ya upelelezi kuonekana unachelewa, rushwa, uhalifu, dalili za viashiria vya ugaidi, ndiyo ayasimamie,"amesema.

Amemtaka Kamishna Haji kuangalia na kusimamia nidhamu ya muda,  fedha na mali za umma.

"Mtu yeyote ambaye unamuona hana uzalendo, askari yeyote ambaye unaona hana maadili chukua hatua, hatua zetu kama huendani na maadili ya kazi tunakufukuza, "amesema.

Amesema Polisi wamepewa dhamana kubwa ya kusimamia ya kutenda haki kwa wananchi hivyo wawaheshimu na kutenda haki kwa wananchi.

"Watanzania wanategemea sisi tutende haki kwa watu, tukitenda haki watatuamini na tutafanya kazi yetu vizuri "amesema.

Akizungumzia suala la rushwa IGP amesema suala hilo ni mtambuka"Sisi kama jeshi la Polisi tunajitahidi sana kutoa elimu, madhara ya rushwa na kuchukua hatua tayari mafiosa kadhaa wamefukuzwa kazi sababu ya rushwa,"amesema.

Amesema suala la rushwa linachangamoto na kwamba wanakazi kubwa ya kutoa ya elimu ili kujua kutoa rushwa ni kosa la jinai.

Amesema suala hilo linapande mbili ambapo wananchi wanapaswa kujua kutoa rushwa ni kosa na atakamatwa na kupelekwa mahakamani.

"Sisi huku ndani tunajitahidi sana kwa askari wetu lakini pia kwenye mikutano yetu wasimshawishi askari na mambo ya rushwa, "amesema.

Amesema watahakikisha wanawakamata wanaovunja kanuni na sheria na kuwapeleka mahakamani.

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, John Marco Kaole, amempongeza Kamishna Haji na kwamba afanye kazi kwa uadilifu kama alivyoapa.

"Niwapongeze wote viongozi wa jeshi la Polisi kwa utendaji wenu...tunaapa kwasababu ndiyo wanaopaswa kuangalia hata watumishi wengine,"amesema.

Amefafanua kuwa tofauti yao na watumishi wengine ni kwamba Polisi wanafanya kazi kwa ajili ya maisha ya wengine.

Amesema wajiepushe na ukiukaji wa maadili ili wasilete mgongano wa maslahi.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Zanzibar na kuapishwa kiapo cha maadili wa Umma, Kamishna wa Polisi Zanzibar(CP),Mohamed Hassan Haji amesema atatekeleza vipaumbele alivyopewa na IGP, Simon Sirro ili watanzania waishi na kupata haki zao inavyostahili.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna wa Polisi (CP), Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search