Sugu, Masonga waachiwa kwa dhamana....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Mbeya
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Jongwe" pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga wameachiwa kwa dhamana.
Wanakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Sugu na Masonga wamekaa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na...
hoja za upande wa Jamhuri.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya hakimu mkazi Mbeya, Michael Mteite leo amewaachia kwa dhamana baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.
Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.
Hakimu Mteite amekubaliana na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.
"Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.
No comments:
Post a Comment