Wafungwa wateka wafanyakazi wa gereza ...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
WAFUNGWA wamechukua udhibiti wa gereza kwenye mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil na baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo wanashikiliwa kama mateka.
Polisi waliojihami wanalizunguka gereza hilo lenye msongamano wa wafungwa la Japari ambalo liko chini ya udhibiti wa genge moja la wahalifu lenye guvu nyingi mjini humo.
Wafungwa watatu ambao walihusika katika kulidhibiti gereza hilo wamepigwa risasi lakini hawajapata majeraha ya kuwatishia maisha.
Ghasia hizo zinatokea siku mbili baada ya rais wa Brazil, Michel Temer, kusaini sheria ya kuwapa wanajeshi ruhusa ya kusimamia usalama wa mji wa Rio de Janeiro.
Maafisa wa gereza wanasema ghasia hizo huenda zimechangiwa na hatua mpya za ulinzi.
No comments:
Post a Comment