Tetesi za soka Ulaya leo Jumapili... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
KIUNGO wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 26, ambaye yuko kwenye mkataka huko Manchester City hadi mwaka 2023, atakamilisha taaluma yake akicheza katika ligi kuu kwa mujibu wa ajenti wake. (Sun on Sunday)
Kevin de Bruyne, 
Kipa wa England na Stoke Jack Butland, 24, anawinda na Liverpool na Arsenal wa kima cha paunia milioni 40. (Sun on Sunday)
Chelsea wanataka meneja Antonio Conte kuondoka klabu hiyo msimu wa joto wakati wa kumalizika mkataba wake, badala ya kumfuta kazi sasa. (Sunday Telegraph)
Everton wanamlenga meneja wa Shakhtar Donetsk kuchukua wajibu wa meneja wa sasa Sam Allardyce msimu wa joto. (Mail on Sunday)
Manchester City wamekubali mkataba wa pauni milioni 50, kumsaini kiungo wa kati raia wa Brazil Fred kutoka Shakhtar Donetsk 24, msimu ujao. (Sunday Mirror)
Liverpool wameanza kummezea mate wing'a wa Bayer Leverkusen' raia wa Jamaica Leon Bailey. (Sunday People)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewambia Real Real Madrid kuwa kipa wa Uhispania David de Gea, 27, haondoki klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Mshambuliaji raia wa Brazil Roberto Firmino, 26, anasema huenda akasalia katika klabu ya Liverpool kwa muda mrefu. (Esporte - in
Tottenham wana uhakika kuwa Mauricio Pochettino atabaki kuwa meneja wao licha ya Real Madrid kummezea mate. (Sunday People)
Mshambuliaji raia wa Algeria Islam Slimani, 29, anatajia kuindoka Leicester kwenda Newcastle kwa mkataba wa kudumu. (Leicester Mercury)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search