Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mashirika ya kimataifa
KLABU ya AC Milan na Inter Milan wana nia ya kumsaini mshambuliaji Mario Balotelli (27) ambaye sasa anachezea timu ya Nice. Raia huyo wa Italia amekasirishwa kwa kupewa kadi ya njano wakati akimlalamikia refa kuhusu kisa cha ubaguzi wa rangi. (Sun)
Mario Balotelli
Kiungo wa kati ya Manchester United, Paul Pogba ( 23) amerejea kwenye mazoezi baada ya kuwa mgonjwa kabla ya mechi ya Jumamosi ya kombe la FA. Man United walipata ushindi dhidi ya Huddersfield. (Mail)
Mchezaji wa Chelsea mbelgiji, Eden Hazard (27) anasema yuko na furaha huko Stamford Bridge lakini hajakata kuwa hatohama klabu hiyo siku za usoni. (Telefoot - in French)
Meneja wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti hafikirii kurudi Paris St-Germain kwa sababu anataka kurudi kwenye Ligi ya Premier (Mirror)
Leicester wametuma maajenti kumtazama beki wa Benfica, Andre Almeida (27) na winga Rafa Silva ( 24). Wachezaji wote hao walihusishwa na Leicester mwezi Januari. (O Jogo via Leicester Mercury)
Meneja wa West Bromwich Albion, Alan Pardew ana mechi mbili za kuokoa kazi yake. (Sun)
Paris St-Germain wanafikiria kutumia pauna milioni 30 kumsaini mlinzi wa Manchester United, Marcos Rojo (27). Mkataba wa raia huyo wa Argentina huko Old Trafford unafikia mwisho msimu ujao. (Sun)
No comments:
Post a Comment