TGNP waandaa kongamano la wanawake na uongozi...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Karoli Vinsent, Dar es
Salaam
MTANDAO wa Jinsia (TGNP)
wameandaa kongamano la Wanawake na Uongozi kwa ajili ya kutoa fursa
kwa wanawake waweze kujitafakari na kujitathimini.
Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa (TGNP) Lilian Liundi akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaamm, Mkurugenzi mtendaji wa (TGNP) Lilian
Liundi amesema Kongamano hilo litatoa fursa kwa wanawake na wadau
wengine kujitafakari ,kutathimini,kusherekea na kupanga mikakati ya kuimarisha ushiriki
wa wanawake katika uongozi.
Amesema Kongamano hilo
litawakutanisha wanawake Viongozi na wadau wengine wa masuala ya usawa wa
kijinsia.
"Tutakuwa na
michango ya wanawake katika nyanja mbali mbali za maendeleo,kushirikishana
uzoefu,changamoto na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana nazo changamoto
zinazowakabili wanawake"Amesema Liundi.
Amesema Kongamano hilo la
litafanyika siku ya jumanne tarehe 27 Februari 2018 katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam na katika Kongamano hilo linatarajiwa
kukutanisha washiriki 250 wakiwemo baadhi ya viongozi.
"Katika Kongamano hili
kutakuwepo na viongozi wanasiasa wastaafu,viongozi wanawake na wanaume walioko
madarakani hivi sasa, wabunge na madiwani,pamoja asasi za kiraia ,wawakilishi
kutoka serikalini"Ameongeza kusema .
Hata Hivyo, Liundi amesema
katika kongamano hilo kutakuwa na fursa ya kipekee ya kutafakari kuhusu kazi
zisizo kuwa na kipato ikiwemo Kulea familia ,wazazi ,wagonjwa ,watu wanaoishi
na Ulemavu.
"TGNP mtandao
tumetoa wito kwa serikali kuanza kutambua na kuthaminisha kazi hizi ili iweze
kuingia katika Pato la Taifa,kazi hizi zinamchango mkubwa katika kukuza uchumi
wa Taifa"amesema
No comments:
Post a Comment