Tetesi za soka Ulaya leo Jumapili....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
KIPAwa Manchester United na Uhispania David de Gea anataka mshahara wa paunia 350,000 kwa wiki ili kusalia huko Old Traford.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 27 analipwa pauni 180,000 kwa wiki laki yuko nyuma wa Mchile Alexis Sanchez, anayelipwa pauni 505,000 kwa wiki. (Sun on Sunday)
David De gea
Mlinzi wa Manchester City Aymeric Laporte, 23, anasema alikuwa sawa kukataa ofa ya kwanza kutoka kwa viongozi hao wa Premier League miezi 18 iliyopita. (Sunday Telegraph)

Mshambualiaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26, amewaambia Real Madrid kuwa anataka pesa zaidi kuliko za mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo ili aweze kuhamia Bernabeu. (Sunday Express)
Kiungo wa kati mfaransa Paul Pogba yuko tayari kuondoka Manchester United ikiwa meneja Jose Mourinho ataendelea kuwepo Old Trafford. (Sun on Sunday)
Manchester United ni kati ya vilabu vikuu vinavyomtazana kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia, Sergej Milinkovic-Savic, ambaye ambaye thamani yake huenda ikawa pauni mioni 80. (Sunday Mirror)
Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal, huenda akachukua mahala pake Antonio Conte, huko Chelsea ikiwa uhusiao wake na Chlesea utazorota zaidi. (Sunday Mirror)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atawanyima wachezaji wake sherehe ikiwa watashinda mechi ya kombe la Carabao leo Jumapili kwa sababu anataka wawe hali nzuri kwa mechi ya Alhamsia dhihi ya Arsenal huko Emirates. (Independent on Sunday)
Chelsea na Crystal Palace wametofautiana kuhusu njia bora ya kumtendea kiungo wa kati aliye na jeraha Ruben Loftus-Cheek.
Mchezaji huyo wa miaka 22 ambaye yupobkwa mkopo huko Palace amekuwa nje tangu mwezi Disemba. (Daily Star Sunday)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez hana hofu kuhusu jereha la mshambuliaji Islam Slimani ambalo huenda likamweka nje hadi mwezi ujao. (Chronicle)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search