Video: Hivi ndivyo Trump Anavyochezesha 'Karata zake Mwenyewe' kuwatumbua Wateule wake.. #SHARE. halafu fuatilia kisa cha kusisimua cha James Corney wa FBI..

..anasimulia Bw. James Corney katika waraka mrefu aliousambaza asubuhi hii akisubiri kuhojiwa na kamati maalum ya Bunge la Sanate la Marekani.. "..James do you still want your job as FBI Director? alianza Rais Trump katika kikao cha wawili hao alichokiita 'diner meeting' kilichofanyika Ikulu ya Rais..  

Corney aliekuwa kwenye mshangao asijue la kufanya, alimeza funda la kahawa, kisha akajibu kwa mkato.. ".. yes indeed, I love my Job", akimaanisha 'ndio boss, bado naipenda sana kazi yangu..'


"..Trump aliniangalia kisha akaniuliza tena.. hivi unafahamu kuna watu zaidi ya kumi wanaitaka kazi yako..?" baada ya hapo,.. anasimulia Corney "..ukimya ulitawala na ndipo maongezi mengine yakatawala huku, lawama na fedheha za wazi dhidi yangu zikaendelea kutoka kwa rais... huku akinihusisha na hujuma na siasa za majitaka katika utawala wake.. kwa kifupi nilimjibu Rais Trump ya kwamba sifungamani na mrengo wowote kisiasa, na ndoto yangu ni kumaliza miaka yangu kumi nikiwa nawe kama Mkurugenzi wako wa FBI..." 


Matukio blog tumekuwekea video ya fupi ya yaliyomo ndani ya waraka huo mrefu, na tutaendelea kukujuvya yatakayojiri kesho baada ya Corney kuhojiwa na Kamati maalum ya Seneti.



___________________________________________
================================
flashbck...dd 7th June, 2017

Jana tarehe 07/06/2017 Rais wa Marekani Bwa Donald Trump, alitangaza nia amemteua na kumtangaza Bw. Christopher Wray kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bw. James Corney aliemtumbua hivi karibuni.

Akibithitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twiter, amesema hana mashaka ya 'Kiithibati' na Bw. Christopher, na kwamba anaamini amepata chaguo sahihi kwa nafasi ya Shirika hilo kuu kabisa la Ujasusi Duniani.
Bw. Wray, ni Mwanasheria aliebobea na mmiliki wa kampuni ya mawakili ya  King & Spalding, aliwahi pia kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu Msaidizi wakati wa utawala wa George W. Bush.

Christopher Wray - mteule mpya wa Trump 
Miezi kadhaa tu tokea rais Trump kuingia Madarakani, kumekuwa na chagizo nyingi kutoka kwa wateule wake. 

Itakumbukwa ni jana tu Mwanansheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions nae alielezea hadharani nia yake ya kujiuzulu kufuatia mahusiano yaliyodorora na bosi wake kwa madai ya kuruhusu kuvuja taarifa muhimu wakati wa kampeni ya Bwana Trump 

Bloomberg magazine&CNN

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search