Uamuzi kesi ya Halima Mdee mwezi Machi....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi Mosi,2018 itatoa uamuzi kama maelezo ya onyo yaliyotolewa polisi na mbunge wa Kawe(Chadema), Halima Mdee yapokelewe kama kielelezo ama la.


Halima Mdee

Ni katika kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli  inayomkabili mbunge huyo.

Hatu hiyo imefikiwa mara baada ya shahidi wa upande wa mashtaka D/SSGT Albogast  kuomba kuyatoa maelezo hayo ya onyo mahakamani kama kielelezo na wakili wa utetezi, Peter Kibatala kupinga kwa madai kuwa yalichukuliwa nje ya muda.

Hakimu Mfawidhi,Victoria Nongwa baada ya kusikiliza pande hizo mbili, Machi Mosi, 2018 atatoa uamuzi kama maelezo hayo ya onyo yapokelewe ama yasipokelewe kama kielelezo.

Halima anadaiwa kuwa Julai 3,2017 katika makao makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni alitumia lugha ya matusi dhidi ya rais Magufuli.

Kwa  kumtukana rais John Magufuli  kuwa“anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search