Usafiri reli ya kati kuanza Machi mosi..... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Reli Tanzania(TRL)imerejesha huduma za usafiri wa abiria Dar es Salaam hadi bara kuanzia Machi 02,2018.
kaimu Naibu Mkurugenzi TRL, Focus Makoye akisisitiza jambo wakati akizungumzia urejeshwaji wa huduma za treni kwa safari za Dar es Salaam hadi Bara.
Huduma hiyo ilisitishwa Januari mosi, 2018 kufuatia mvua kuharibu miundombinu ya reli eneo la Kilosa na Gulwe na kusababisha kupata hasara zaidi ya sh. bilioni 1.6.
Kaimu Naibu Mkurugenzi TRL, Focus Makoye amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa marekebisho ya miundombinu ya reli imekamilika.
"Uamuzi huu wa kurudisha huduma kuanzia Dar es Salaam umetolewa na kampuni baada ya kufanya tathmini ya ukarabati uliofanyika kwa kipande hicho cha reli kati ya Kilosa na Gulwe, "amesema.
Amesema tayari treni za mizigo 30 zimeshapita katika eneo hilo bila ya matatizo.
"Treni yetu ya kwanza inatarajia kuanza safari zake ijumaa saa tisa alasiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro, Dodoma, Tabora na Kigoma.Treni zitaendelea na safari zake kama ilivyokuwa awali.
"Treni ya abiria inayotarajia kuondoka leo Katika kituo cha Dodoma kuelekea Tabora na Kigoma, treni hiyo itatoka Kigoma Machi mosi, 2018 na kuja moja kwa moja Dar es Salaam, "amesema.

No comments:
Post a Comment