TANNA walaani muuguzi kupigwa....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
Chama Cha Wauguzi Nchini (TANNA) kimelaani
tukio la shambulio la muuguzi lililotokea Februari 18, 2018 katika
Hosptali ya Bugando jijini Mwanza na ndugu wa mgonjwa ambaye muuguzi huyo
alikuwa akimuhudumia na kufariki dunia.
Makamu wa rais wa TANNA Dk. Ibrahim Mgoo, amesema kabla ya shambulio hilo muuguzi alitimiza wajibu
wake wa kazi , alishambuliwa na watu wanaojulikana waliokuwa na kusudi la kutoa
uhai katika chumba cha uangalizi maalumu (HDU), Hospitalini hapo, ambapo ni
kinyume na taratibu za hosptali hiyo.
“Kabla ya mauti kumfika mgonjwa huyo ndugu
zake walilazimisha wabaki katika chumba hicho jambo ambalo, halikukubaliwa na
muuguzi huyo, kesho yake walipotaarifiwa ndugu yao amefariki, ndipo walipoamua
kufanya kitendo cha unyama na udhalilishaji kwa kumshambulia na kumjeruhi
muuguzi alipokuwa anatoa huduma kwa wagonjwa wengine”, alisema.
Makamu Mgoo, ameviomba vyombo vinavyohusika
kuchukua hatua stahiki, kwa wahusika mapema ili kutoathiri utendaji wa wauguzi
nchini, ikiwa ni pamoja na kuboresha ulinzi wa wauguzi na watumishi wengine
mahala pa kazi ili kutoleta madhara makubwa katika kazi.
Aidha, ametoa shukrani kwa hatua
zilizochukuliwa na uongozi wa Hospitali ya Bugando ukishirikiana na chama cha
wauguzi, kuhakikisha Muuguzi huyo anatendewa haki katika vyombo vinavyohusika.




No comments:
Post a Comment