Ushahidi waendelea kutolewa dhidi ya Wema Sepetu... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam

Shahidi wa pili  upande wa mashtaka, Inspekta Wille  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliijaza fomu ya kupima sampuli ya mkojo wa Wema Sepetu ofini kwake kabla Wema hajapimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.


Wema Sepetu

Pia Inspekta Wille  amedai hajawahi kupeleka sampuli za mkojo  za washtakiwa Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas ambao ni wafanyakazi wa Wema kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Shahidi hiyo aliyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba wakati akihojiwa na Wakili wa upande wa utetezi,Albert Msando mara baada ya kutoka ushahidi wake.

Shahidi hiyo amedai  aliijaza fomu ya kupeleka sampuli ya mkojo wa Wema saa nne kamili asubuhi akiwa ofini kwao na kuandika maneno mkojo ndani ya chupa ya plastiki.

Anedai aliijaza hivyo kwa sababu ya uzoefu kwa miaka 15 kuwa  ukifika katika ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali mkojo unakuwa katika chupa ya plastiki.

Aliendelea kudai kuwa Februari 8,2017alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali  saa tano asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo.

Wakili Msando alimuuliza shahidi ulikuwapo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki  unaodaiwa kuwa ni wa Wema  wakati unachukuliwa ambapo Inspekta Wille alidai kuwa hakuwapo.

 Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille anaweza kusema kuwa unajua kwa uhakika kilichokuwa ndani ya chupa ya plastiki kuwa ni mkojo na he ni mkojo wa Wema.  Baada ya kuulizwa hilo, Inspekta Wills alidai kuwa yeye hajui.

Msando alimuhoji Inspekta Wills kuwa walikaa kwa muda gani katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Inpekta Wille alidai kuwa hakumbuki.
Shahidi huyo alidai kuwa yeye hakupekuwa katika chupa anacholala Wema bali alipekuwa katika chumba anachohifadhia nguo ikiwamo nguo na viatu.

Alidai kuwa katika upekuzi walikuta msokoto wa bangi jikoni juu ya kabati, pia walikuta msokoto wa bangi uliotumika ukiwa ndani ya kiberiti dirishani katika chumba wanacholala wafanyakazi wa Wawili  wa Wema.

Hata hivyo walishindwa kueleza msokoto huo ni wanani kati ya wafanyakazi hao wakili wa Wema.

Mahakama iliipokea hati ya ukamataji mali iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 na msanii wa Filamu,  Wema Sepetu  kama kielelezo.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 26 na 27,2018 itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Inspekta Wille awali akitoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo alidai katika upekuzi huo walifanikiwa kukuta misokoto inayodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Wille alidai kuwa Februari 4,2017 anaikumbuka kwa sababu aliitwa na Mkuu wake wa kazi  na kupewa kazi ya kufanya upekuzi  nyumbani kwa Wema na aliongozana na WP Mary, Koplo Robert, PC Hassan na dereva kuelekea Unonio anapoishi Wema ili wakaufanye upekuzi huo.

Inspekta Wille alidai  kuwa walipofika  nyumbani kwa Wema huko Ununio waligonga mlango na  kwamba waliwakuta wasichana wawili ambao ni wafanyakazi  wa Wema  na wakaomba  waitiwe mjumbe wa nyumba kumi Steven Noho wakaitiwa.

Shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka alidai kuwa walimueleza kuwa wamekwenda nyumbani kwa Wema kwa nia ya kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema na wanatafuta dawa za kulevya na kitu chochote ambacho wangekitilia shaka.

Wema alisema dada yake awepo ili ashuhudie upekuzi huo, dada yake alifika na tukapekuwa  ambapo upekuzi wetu ulianzia jikoni  ambapo juu ya kabati la vyombo  tulifanikiwa kukuta msokoto mmoja unaodhaniwa kuwa ni bangi na karatasi ya kusokotea, Alieleza shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka.

Katika chumba cha Wema ambacho anahifadhia nguo na vitu vyake vingine mlango ulikuwa umefungwa lakini wafanyakazi wake walituletea, tukafungua  na tukafanikiwa kukuta vipisi na msokoto unaodhaniwa  kuwa ni bangi dirishani.”Alieleza shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka.

Akiendelea kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo, Inspekta Wille alidai kuwa upekuzi huo uliendelea  katika chumba cha wasichana wa kazi wa Wema, walifanikiwa kukuta kiberiti ambacho ndani yake kulikuwa na msokoto ambao unaonekana  umeishavutwa.

Alidai kuwa baada ya kufanya upekuzi huo, walisaini hati ya ukamataji wa mali ambapo yeye aliisaini,  Wema mwenye aliisaini, wafanyakazi wake, dada yake, pamoja na mjumbe wa eneo la Unonio.

Aliongeza kuwa baada ya hapo walienda kituoni na kumkabidhi mtunza vielelezo, Robert.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.

Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.Awali Wema alikiwa akitetewa na Peter Kibatala ambaye alijitoa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search