Diamond: Wananigombanisha na Amisa Mobeto...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam

MWANAMUZIKI Nasib Abdul 'Diamond Platinum' amesema  watu wenye  nia mbaya wanamgombanisha na mzazi mwenzake Amisa Mobeto kupitia mtoto wao.

Diamond akiwa na mmoja wa watoto wake

Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika eneo la Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kitengo cha watoto mara baada ya kesi yao ya usuluhishi wa malezi ya mtoto wao kusomwa.

"Kiumakini hakukuwa na vita kati yetu sisi wawili, ila kwa upande wa mwenzangu kulikuwa na watu wanaingiza chuki ilimradi kutengeneza mazingira ya kunigombanisha na kumkomoa Diamond kitu ambacho tumeona hakimsaidii mtoto," amesema
Diamond amesema atahakikisha mtoto wake anakuwa katika mazingira mazuri, asome kadri ya uwezo nitakaokuwa nao.

"Kwani maisha ni kupanda na kushuka kuna wakati unakuwa hauna unasema leo mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha ndivyo yalivyo," amesema Diamond na kuongeza

"Hivyo tumekubaliana na tumeyamaliza na tumeweka misingi mizuri ya kumlea mtoto wetu, kwani mwisho wa siku hata mahakama haiwezi kunambia nimlipe Mil.5 nitaitoa wapi, nina kazi mie, Mahakama imenipa kazi au kuna mtu amenipa kazi...? au eti mtoto umjengee nyumba, ulinipa mie nyumba-Diamond."




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search