TECNO kusheherekea krismas,mwaka mpya na wadau...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu,Dar es salaam

KAMPUNI ya simu TECNO mobile Ltd imeandaa sherehe za awali za Krisimas maalum  kwa  wadau wake.

Pia hivi karibuni kampuni hiyo iliwakutanisha wadau na mashabiki wake kutoka katika mitandao ya kijamii ya Twitter, Instagram, Facebook na TECNO spot katika hafla fupi iliyopewa jina la “TECNO Fans Night” iliyofanyika katika uwanja wa burudani wa ESCAPE ONE Mikocheni.

Lengo kuwapongeza na kutoa shukurani kwa wadau na mashabiki kwa kuwa pamoja na kampuni hiyo kwa mwaka mzima na kuwa mabalozi wa kampuni hiyo ya simu.


Hafla hiyo  ilipambwa kwa  michezo, burudani na chakula cha jioni  huku zawadi  mbalimbali zikitolewa

“Kiukweli nimefurahi kuwa hapa, kuungana na wenzangu. Nimepata nafasi ya kuongeza marafiki usiku wa leo, asante sana TECNO” – alisema mmoja wa wadau/shabiki wa TECNO.

“Mpaka sasa kwa mwaka huu tumeweza kuwa na ushawishi sana kwa upande wa mitandao ya kijamii na tumeweza kuwapa kile wadau na mashabiki wetu wanapenda, nahisi ndicho kilichoweza kutupa mabalozi kama hawa. Kiukweli hatuwezi kuwa sisi bila ya watu kama hawa ambao waipenda bidhaa na kampuni hivi, hivyo ni sawa tu kama na sisi kama kampuni tukatenga muda ili kuweza kuungana nao kusherehekea mafanikio na pia sikukuu.”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search