Watanzania watatu, wanaigeria watano mbaroni kwa dawa za kulevya...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
WATANZANIA watatu na raia
watano wa Nigeria wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji wakidaiwa kupatikana na
dawa za kulevya zikiwamo Heroin, Cocaine, bangi na mashine ya kutengeneza dawa
hizo.
Dawa za kulevya
Kaimu Kamishna wa Usimamizi na
Udhibiti wa Mipaka, Kagimbo Hoseah amesema watuhumiwa wamekamatiwa eneo la
Masaki jijini Dar es Salaam
.
Hoseah amewataja Watanzania
kuwa ni Ruth Kabezi, Lucy Adolf na Lizzy Minja ambaye ni wakili wa kampuni ya
Law Associates.
Wanigeria wametajwa kuwa ni,
Bisola Adeyemi, Olasunkanmi Kayode, Aaron Ejeh, Obina Nwauba na Darlington
Nwauba.
“Tunaendelea
na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, tutakapokamilisha
hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kuwafikisha mahakamani,”
amesema Hoseah.
No comments:
Post a Comment