CCM yashinda Siha....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa marudio jimbo la Siha mkoani
Kilimanjaro Dk. Godwin Molel ametangazwa kuwa mshindi.
Dk. Godwin Molel akikabidhiwa cheti cha ushindi wa ubunge jimbo la Siha
Akitangaza matokeo msimamizi wa
uchaguzi wa jimbo hilo Valerian Juwal, amesema kuwa Dk. Molel amepata kura
25611 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Elvis Mosi aliyepata kura 5905.
Mgombea wa Chama cha Wananchi
CUF Tumsifuel Mwanri amepata kura 274 huku wa Chama
cha SAU Azaria yeye akipata kura 170.
No comments:
Post a Comment