Waziri Mwigulu awaonya askari magereza....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Geita

WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi, Dk Mwigulu Nchemba  amewataka askari wa jeshi la magereza kufanya kazi kwa weledi na kufata maadili ya kazi.

Waziri Nchemba akifungua gereza wilayani Chato mkoani Geita

Waziri Dk Mwigulu meyasema hayo akifungua gereza la wilaya ya Chato mkoa wa Geita jana.

Amesema kuna taarifa ya baadhi ya askari wanaokiuka maadili ya kazi na masharti ya wahalifu wawapo magerezani kwa kushirikiana nao kwa kuwapa simu na vitu vingine ambavyo ni kinyume cha sheria na maadili ya kazi yao.

Amesema sasa majira yamebadilika na aina ya wahalifu wamebadilika ni wajibu wa askari kuzingatia maadili ya kazi kuliko walivyokuwa wakifanya zamani enzi watanzania wote wakiwa ndugu na wahalifu.

"Kuna taarifa za rejareja za baadhi ya magereza vijana wetu wanawapa simu wafungwa kuwasiliana na jamaa zao, zamani unaweza fikilia anasalimia familia lakini si sasa unaweza mpa simu kumbe anapanga mpango wa kuwateka, majira yamebadilika. Sheria zipo basi tuzingatie sheria na maadili ya kazi zetu".alisema Dk Mwigulu.

Waziri huyo amesema  magereza yajengwa ili kusaidia  wanaopata matatizo lakini serikali inataka watu wasifanye makosa kupelekwa magerezani.

Mkuu wa jeshi la magereza, kamishna jenerali wa magereza Dk. Juma Malewa amesema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo baada ya kufungua gereza  ni usafiri, upungufu wa askari  na wanapofungua gereza jipya huitaji askari wasiopungua 50 na changamoto nyingine ni miundombinu chakavu ya magereza

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Geita, Eng. Gabriel Robert amesema mkoa umejipanga kuhakikisha wanatoa ardhi kwa jeshi la magereza kwa ajili ya kilimo na ufugaji ili lijitegemee
 katika chakula na kiuchumi


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search