Mke Tsvangirai kutohudhulia maziko ya mume wake....soma habari kamili na matukio360....#share


Na mashirika ya kimataifa
WAKATI leo mchana kiongozi wa chama cha MDC, Morgan Tsvangirai atazikwa kijijini kwao Buhera, mke wake Elizabeth Macheka, hatokuwepo.

Hatua hiyo inatokana na kupoteza fahamu kutokana na presha kupanda na familia kulazimika kumuacha mjini Harare na kuzuia asishiriki maziko hayo

Jeneza lenye mwili wa Morgan Tsvangirai
Jana majira ya mchana mamia ya Wazimbabwe walitoa heshima za mwisho kwa kuuaga mwili wa kiongozi huyo katika viwanja vya shule ya msingi Makanda.


Mwili wa Tsvangirai uliwasili hapo kwa helkopta mbili  za jeshi la Zimbabwe, ukishindikizwa na mama mzazi wa kiongozi huyo, Mbuya Lydia Chibwe Tsvangirai, kaka yake Collin na mtoto wake Edwin.
Makamo mwenyekiti wa MDC, Messrs Nelson Chamisa na Elias Mudzuri ambaye anatarajiwa kuongoza chama hicho hawakupanda helkopta hizo.

Mama wa Morgan alilazimika kumzuia Elizabeth asihudhulie maziko, akihofia anaweza kupoteza maisha.

Morgan Tsvangirai alifariki hivi karibuni nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa kansa ya utumbo.

Miongoni mwa viongozi watakaohudhulia maziko hayo ni rais wa Zimbabwe, Emerson Mnagangwa na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search