Waziri Nchemba aagiza wakimbizi 34000 warejeshwe Burundi...soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Ngara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewaagiza shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia (UNHCR) kuwaondoa wakimbizi 34000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.
Waziri Nchemba akipewa maelezo mbalimbali kuhusu wakimbizi
Amesema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendelea katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mara moja.
Dr Mwigulu amesema UNHCR wanafanya kazi saa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini mwao.
"Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanahitaji kurudi makwao,naagiza muwaandikie barua leo hii kuwa hao wakimbizi ambao wapo katika kambi za Nduta, Nyarugusu na mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanahitaji kurudi kwao wakajiletee maendeleo," amesema Mwigulu
Waziri huyo amesisitiza kuwa kwa hakutakuwa na kikao cha pande tatu kujadili uondokaji wa wakimbizi kwa kuwa hilo lilifanyika mwaka jana na kwamba mwezi huu ni wa kilimo
na kuwapeleka mwezi wa nne itapelekea waishi maisha magumu zaidi.
Naye mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma, Tonny Laizer amesema kutokana na hali ya usalama nchini Burundi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutopokea waomba hifadhi, kituo cha Lumasi kinafungwa na serikali ya wilaya itakabidhiwa na UNHCR kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

No comments:
Post a Comment