Bilioni 1.7 zatumika ujenzi vituo vya afya....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu,Mbeya. 



SERIKALI imetoa zaidi ya sh bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vitatu katika kata za Ilembo, Santilya na Ikukwa halmashauri ya Mbeya Vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makall, wa pili (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Aran Njeza mwenye miwani wakiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Ilembo.


Mganga Mkuu wa wilaya , Lauis Chomboka amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Ilembo kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, utakaogharimu sh milioni 400.


Amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa maabara, jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, wodi ya watoto, nyumba ya  mtumishi,chumba cha kuhifadhia maiti, mfumo wa kukusanyia maji na sehemu ya kuchomea taka..

Amesema zahanati hiyo itahudumia vijiji 10 vyenye wakazi 17,166 kati ya hao, wanawake 9,278 na wanaume 8,888 na kwamba idadi ya wanawake wanye uwezo wa kushika mimba ni 3, 777 .

Chomboko amesema kituo cha afya ilembo kina watumishi 32 na kina upungufu wa watumishi 21 wa kada mbalimbali na kuomba serikali kuongeza watumishi.


Kaimu Mganga Mkuu, Yahya Msuya amesema katika mpango wa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya,kati ya vituo 44 katika halmashauri 82, mkoa wa mbeya ulipata vituo viwili katika halmashauri ya Rungwe kituo cha afya Ikuti na kituo cha afya Ipinda wilayani Kyela.


" Kutokana na kufanya vizuri katika ujenzi wa vituo vya afya Rungwe na Kyela katika awamu ya pili kati ya vituo vya afya 139 nchi nzima mkoa wa mbeya umepata vituo sita na katika hatua za awali tumeanza na vituo vya afya Ikukwa,Santilya na Ilembo ambavyo vitagharimu Sh bilioni 1.7,"amesema.

Mkuu wa mkoa Amos Makalla ameagiza watumishi wa afya katika halmashauri na ofisi ya mkoa kuelekeza nguvu ya utendaji kazi katika ujenzi wa kituo cha afya Ilembo na ifikapo Mei 30 mradi ukamilike.


"Kuna watu wamekaa tu maofisini sasa ninaagiza kuanzia sasa waweke kambi huku ilembo ili kusukuma kasi ya ujenzi wa mradi huo na ujengwe kwa ubora wa hali ya juu ili jamii iweze kupata huduma bora za afya ya msingi hususan upasuaji na kuacha kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya," amesema.

Katika hatua nyingine Makalla amewaonya wanaopita kwa wananchi kuwashawishi kutoshiriki katika shughuli za miradi ya maendeleo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search