Afya ya Aveva wa Simba yaanza kuimarika.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abdulrahim Sadiki Dar es Salaam.
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Kisutu imeelezwa kuwa afya ya rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva imeanza kuimarika na Aprili 5, 2018 mahakama hiyo itawasomea maelezo ya awali Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange 'Kaburu' .
Evans Aveva kushoto akiwa na Godfrey Nyange
Ni baada ya Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kueleza mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na akaomba ipangiwe tarehe kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali (PH).
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Wakili anayewatetea washtakiwa hao,Steven Mwakibolwa aliiambia mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na kwamba hali ya Aveva inaimarika ila siyo nzuri sana. Aveva anasumbuliwa na ugonjwa wa figo na amelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili (MNH)
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye kesi hiyo kwa sasa itasikilizwa mbele yake badala ya Hakimu Victoria Nongwa aliyekuwa akiisikiliza awali, alisema kama hali ya Aveva itakuwa imetengemaa kesi hiyo wataisikiliza mfululizo.
Alisema kesi hiyo ilifunguliwa Juni 26,2017 na watajitahidi isikilizwe na kumalizika ndani ya miezi 12.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.
Washtakiwa hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment