Askari JWTZ asomewa mashtaka ya mauaji akiwa kitandani....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu Dar es Salaam.
MWANAJESHI MT 109795 Private Ramadhan Mlaku (28) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la mauaji ya askari mwenzie, MT 79512 SGT Saimon Munyama.
Mshtakiwa hiyo amefikishwa mahakamani leo na gari la kubebea wagonjwa la JWTZ.
Nyakati za saa sita mchana alishushwa ndani ya gari hilo akiwa katika kitanda cha wagongwa na kupelekwa katika chumba cha mawakili wa Serikali na kusomewa
shtaka linalomkabili.
Akisomewa shtaka na Wakili wa Serikali,Mosii Kaima mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba alidaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 30,2017.
Imedaiwa mshtakiwa huyoo ambaye ni Mwanajeshi wa kambi ya Jeshi la Makongo siku hiyo ya Oktoba ,30,2017 akiwa Makao Mkuu ya JWTZ Upanga Ilala Dar es Salaam alimuua askari mwenzie MT 79512 SGT Munyama.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa hiyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo.
Pia kosa hilo halina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Upande wa mashtaka umedai upelelezi bado haujakamilika na hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kujitahidi kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo mapema.
Kesi imeahirishwa hadi Machi 28,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi itakuwa umekamilika ama la.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa hiyo alipandishwa tena katika gari la Jeshi la Wagonjwa na kupelekwa mahabusu.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment