Milioni 700 kutumika ujenzi kituo cha afya, ununuzi vifaa tiba....soma habari kamili na matukio360...#share






Na mwandishi wetu,Mbeya.


SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEM) imetoa milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa katika kituo cha afya cha Ruanda mkoani Mbeya huku milioni 200 zitatumika katika ununuzi vifaa tiba.


Amos Makalla

Akizungumza na matukio360, mkuu wa mkoa huo Amos Makalla amesema serikali imeguswa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya afya hususan ujenzi wa vituo vya afya na zahanati lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za wadau wanaojitolea kuchangia hususan Taasisi ya Tulia Trust.

"Napongeza jitihada za wadau ndio zimeleta chachu katika
mkoa wangu.Pia kuna fedha zilitolewa na Serikali kwa ajii ya
kuboresha kituo cha Afya Ilembo kilichopo mbeya vijijini na Ikuti
Wilayani Rungwe,"amesema.

Amesema jamii inawajibu wa kuchangia shughuli za miradi ya
maendeleo ili kuunga mkono jitihada za serikali na kwamba serikali bado itaendelea kuchangia miradi hiyo hususan majengo ya upasuaji,wodi za wazazi na watoto kuhakikisha wanapata huduma muhimu na salama.

"Wananchi nanyi mnalojukumu la kusaidiana na serikali katika kusukuma mbele miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha ifikapo 2020 kila kijiji na kata kunakuwa na kituo cha afya na zahanati na kuwapuuza wanaopita kuwalaghai,"amesema.

Makalla ameonya wanasiasa kuachana na dhana ya kupotosha jamii kutochangia miradi ya maendeleo na badala yake usiasa uwekwe pembeni na kuleta maendeleo," amesema.

Wakati huo huo Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Ruanda , Elioth Sanga amesema Sh 55 milioni zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upasuaji.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search