Bilioni 1.5 kujenga kituo kumbukumbu za historia...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

SERIKALI imetenga sh bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu cha kumbukumbu za historia za ukombozi wa nchi za bara la Afrika.

Makao makuu ya Kamati ya Ukombozi wa OAU, yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam,jengo hilo linatarajiwa kufanyiwa maboresho ili libaki kama kumbukumbu

Ujenzi huo utashirikisha nchi za kusini mwa Afrika(SADC) na kitajengwa Mabwepande, hekta 50 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Kamati Ukombozi ya OAU,  na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo,  Dk Harrison Mwakyembe wakati alipotembelewa na Balozi wa Shirikisho la Urusi, Yuri Popou.

“Uchaguzi wa tujenge wapi makao makuu ya kumbukumbu ya ukombozi wa bara la Afrika yawe Dar es Salaam hatukuamua sisi, waliamua wakuu wa nchi za Afrika(AU) kwenye kikao chao kilichofanyika Adis Ababa,”amesema.

Amefafanua kuwa walitaja mkoa huo kwa kukumbukumbu ya mchango ambao ulitoa kwa kuwa mwenyeji wa Kamati ya Ukombozi wa OAU iliomalizia kazi yake 1994 Posta.

 "Lakini tumegundua  eneo hilo ni dogo,si tu kumbukumbu  pia kitakuwa ni kituo cha Tehama na kubadilishana taarifa habari za kumbukumbu na kitengo cha nyaraka za kale,maktaba kubwa itakayokusanya vitu vingi vikubwa," amesema

Mwakyembe amesema tayari wameshakamilisha upatikanaji wa hati Wizara ya Ardhi na mwishoni mwa mwezi huu mawaziri wa utamaduni wa nchi za kusini mwa Afrika watakutana nchini Tanzania


“Mradi huu unasehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa kituo kikuu kwa ajili ya bara la Afrika ndiyo hiyo ya Mabwe pande lakini kila nchi inahistoria ya kumbukumbu ya ukombozi nayo inahitaji kuwa na kituo chake cha nchi.

Akizungumzia Ujio wa Blozi Popou, Mwakyembe amesema bado kuna kumbukumbu za mchango wa Urusi katika ukombozi wa bara la Afrika

“Tumekuta pikipiki aliyokuwa akitumiwa na aliyekuwa Kiongozi wa Msumbiji wa Samora Michele, “amesema.

Pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Msumbiji, Samora Michele ikiwa imebaki kama kumbukumbu kwenye makao Makuu ya iliyokuwa Kamati ya Ukombozi,  OAU

 Balozi wa Shirikisho la Urusi, Yuri Popou alipotembelea yaliyokuwa Makao Makuu ya Kamati Ukombozi ya OAU, amempongeza Waziri Mwakyembe kwa kupata nafasi ya kuonana nae na kuahidi kushirikiana kujenga kituo hicho.

“Nimefurahi kuonana na Waziri…Rusia ilikuwa ni sehemu ya upatikanaji wa uhuru wa Afrika na mafanikio hivyo ni hatua kubwa kujenga kituo hicho,”amesema

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search