Upelelezi mauaji ya mkurugenzi bado haujakamilika.....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mwandishi wetu Dar es Salaam.
UPELELEZI wa kesi ya mauji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, Wayne Lotter inayowakabili washtakiwa saba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
UPELELEZI wa kesi ya mauji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, Wayne Lotter inayowakabili washtakiwa saba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
Hayo yameelezwa jana na wakili wa Serikali, Adolf Mkini kwa Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hata hivyo mahakama ilielezwa na mshtakiwa Rahma Almas kuwa mshtakiwa
Mohammed Maganga anaumwa.
Wakili Mkini aliieleza Mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hadi Machi 21,2018 kwa ajili ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Washtakiwa wanakabiliwa na kesi hiyo ni raia wa Burundi, Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) Mkazi wa Kamenge Burundi na Mfanyabiashara Godfrey Salamba (42) Mkazi wa Kinondoni Msisiri A.
Wengine ni Mfanyabiashara Inocent Kimaro (23) Mkazi wa Temeke Mikoroshini, Mfanyabiashara Chambie Ally(32) Mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa Benki ya NBC, Robert Mwaipyana (31) Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo katika shtaka la kwanza wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16,2017 wakiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao na wenzake watatu walikula njama ya kufanya mauaji ya Wayne Lotter.
Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni DSM, walimuua Lotter.
Washtakiwa hao, wameunganishwa na washtakiwa watatu waliokuwa wanakabiliwa na kesi hiyo awali ambapo kesi yao ipo katika hatua ya kutajwa kwa sababu upelelezi wake bado haujakamilika.
Washtakiwa hao ni Meneja wa Benki ya Baclays Khalid Mwinyi (33) Mkazi wa Mikocheni B, Mfanyabiashara Rahma Almas (37) Mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment