Dawati za kijinsia kuwepo maofisini....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


MWENYEKITI wa Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Rehema Ludanga amesema hadi kufikia mwaka 2025  madawati ya kijinsia mahala pa kazi yatakuwepo.

Hatua hiyo  inafuatia vitendo vya unyanyasaji wa kijinisa mahala pa kazi kuendelea kukithiri  nchini huku asilimia 30 ya wanawake wafanyakazi  wakikabiliwa na unyanyasaji huo.



Mwenyekiti Kamati ya wanawake, Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini(TUCTA),Rehema Ludanga (katikati) akisistiza jambo juu ya kongamano la wanawake litakalofanyika Machi 7/2018 kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Ludanga ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani Machi 8/2018 na wanatarajia kufanya kongamano la wanawake Machi 7,2018 lengo kujadili na kutoa tathmini ya unyanyasaji wa kijinsia mahala pa kazi.

Amesema unyanyasaji huo umekuwa ukizungumzwa na wanaharakati wengi, hadi sasa hakuna tathmini inayoonesha walipotoka na wanapoelekea.

"Tumeona tutumie maadhimisho haya  kutathmini, kuona tulipotokea, tulipo na tunapokwenda  na kuona changamoto zinazokabili wanawake,"amesema.

Amesema kongamano hilo litajadili na kufikia hatua wanayoitaka kwani wanawake wamekuwa katika kundi ambalo halipo sawa na wanaume.

"Tumejitahidi sana kuwaelimisha, je watu hawafahamu? Kwa nini inaendelea hivyo Machi 7,2018 tutatumia kongamano hili kujadili suala hili, hapo tutaelewa wapi tulikwama ili ifikapo 2025 liwe historia, "amesema.

Amesema wanawake wamekuwa wakinyanyaswa mahali pa kazi kwa kukosa vipaumbele kutokana na majukumu yake kama uzazi.

"Suala unyanyasaji lipo na kwa kiwango kikubwa...Tunatakiwa kuendelea kupambana ili uishe kama si kupungua, "amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Vyama vya wafanyakazi Tanzania(TUCTA),Yahya Msigwa amesema wanawake wanamahitaji  maalum.

"Lazima tusimame kidete tuweze kuwatetea hawa ni jamii yetu, mama zetu.. . Haki zao lazima zichukuliwe, hata Nyerere alisema jamii yeyote haitapata maendeleo kama inaacha kundi la kina mama nyuma, "amesema.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search