Museveni amtimua kazi waziri wa ulinzi na IGP.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.
Yoweri Museveni
Generali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.
Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama.
Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maeneo yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.
Naibu wake Okoth Ochola anashikilia wadhifa huo.
Kwa mujibu wa ujumbe alioandika rais Museveni katika mtandao wa Twitter, amesema: " Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.
Mnamo Mei mwaka 2017 Rais Museveni alimteua upya Kayihura kama mkuu wa polisi kwa muhula mwingine wa miaka mitatu,hadi mwaka 2020.
Uteuzi huo ulikumbwa na mzozo na haukudumu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search