Jalada kesi mke bilionea Msuya kwa DPP....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu Dar es salaam
Upande wa Mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kulifanyia maamuzi.
Miriam Mrita akiwa katika mahakamani
Miriam Mrita akiwa katika mahakamani
Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alidai leo, Machi 6, 2018, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40) na wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Itakumbukwa kuwa , Februari 21,mwaka huu upande wa mashtaka ulidai Mahakamani hapo kuwa, jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi hii lipo kwa DPP kwa ajili ya kulifanyia maamuzi, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa " alidai Kishenyi.
Baada ya Kishenyi kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala alikubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe fupi.
Kutokana na maelezo ya pande zote, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, mwaka huu, itakapotajwa.
Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji, ambapo wanadaiwa kumuua dada wa Bilionea Msuya, Aneth Msuya.
Februari 23, 2017 , washitakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa shtaka moja la mauaji upya.
Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016, maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment