Jinsi moto ulivyoteketeza soko la mbagala....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


SOKO la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijini Dar es salaam leo limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kwa zaidi ya wafanyabiashara 300 hasa wauza nguo za mitumba.



Moto huo ulioanza asubuhi chanzo chake hakijajulikana hadi sasa ikiwa ni miezi kadhaa tangu kuungua kwa soko hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula amethibitisha kuungua kwa soko hilo na kwamba hakuna madhara ya kifo yaliyotokea.


Kamanda Lukula amesema  moto huo umeteketeza soko hilo kwa saa tatu ña kwamba ulianza majira ya saa moja asubuhi.

"Nilifika eneo la soko saa 1 lakini niliukuta moto ukiwa mkubwa sana  nikawasiliana na kikosi cha zimamoto na kufanikiwa kuudhibiti moto huo kwa saa tatu," amesema na kuongeza chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.



Amesema  baada ya kufanikiwa kuuzima moto  huo kamati ya maafa ya Kata hiyo imekaa kwa ajili  ya kutathmini  watu waliounguliwa pamoja na bidhaa zilizoungua.

Amesema kamati ikimaliza  kutathmini watampelekea na kuitoa hadharani


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search