Jinsi polisi Dodoma walivyowakamata wahamasishaji maandamano....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JESHI la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akiwa amewatazama watuhumiwa wa uhamasishaji wa maandamano.
Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto akizumgumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, amesema watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.
Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria.
"Watu hawa wamekuwa wakihamasisha wananchi kufanya maandamano, tulishasema Serikali haijalibiwi leo tunaanza kutoa mifano kwao. Wale wote wanaoijaribu Serikali tutahakikisha tunawachukulia hatua za hali ya juu sana” amesema
Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment