Barabara Tabora-Itigi yakatika....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Tabora
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa
kuamkia jana katika eneo la Nyahua wilayani Uyui Mkoani Tabora imesababisha
kukatika kwa barabara kuu ya Tabora kupitia Itigi hadi Singida na kusababisha
magari ya abiria na mizigo kushindwa kuendelea na safari zake kwa kutumia
barabara hiyo.
Baadhi ya wasafiri na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakiwa katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora.Nyuma ni basi dogo la Prince Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana katika eneo la tukio Meneja wa Wakala wa Barabara )TANROADS) Mkoa wa
Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze alisema mvua zilizonyesha katika maeneo
hayo zimesababisha kukatika kwa eneo hilo ambapo ndipo barabara ya lami
inaishia.
Aliwataka madereva wa magari ya
aina yoyote kudiriki kupita katika aina hilo kwa sababu wanaweza kuhatarisha
maisha yao na abiria na mizigo.
Ndabalinze alisema dereva yoyote
atakayekaidi na kuamua kupita katika eneo hilo kwa kulazimisha jambo lolote
litakalompata itakuwa ni yeye kajisababishia na asilelekeze lawama kwa chombo
chochote.
Baadhiya wasafiri kutoka katika
Basi la Prince Ramigo na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakijaribu kuvuka
jana katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha
na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora.
Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Damian Ndabalinze akizungumza na
waandishi wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio
ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na
kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian Kamuhanda akizungumza na waandishi
wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua
kubwa iliyonyesha na ku sababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora na kisha kutoa tahadhari kwa Madereva kutodiriki kupita katika
eneo hilo.
Basi la Prince Ramigo
linalosafirisha abiria kutoka Dodoma kwenda Tabora likiwa limekwamwa
katikati ya maji jana mara baada ya Dereva kujaribu kupita.
Picha na Tiganya Vincent
No comments:
Post a Comment