Kesi Malinzi, wenzake sasa kusomewa maelezo ya awali....soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abdulrahim Sadiki Dar es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 11,2018 inatarajia kuwasomea maelezo ya awali (PH )  waliokuwa vigogo watatu wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambao wanasota rumande kwa miezi tisa sasa.

Jamali Malinzi kushoto akiwa na Mwesigwa Joas Selestine

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru),Leonard Swai kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Baada ya kueleza hayo, Swai aliiomba mahakama kupanga tarehe kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali (PH). Ambapo Hakimu Mashauri ameipanga Aprili 11,2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Washtakiwa hao  wakishasomewa maelezo hayo ya awali kesi hiyo itaanza kusikilizwa rasmi kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Vigogo wanaokabiliwa na kesi hiyo ni aliyekuwa Rais TFF, Jamal Emil Malinzi(57), Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27)

Washtakiwa hao walipandishwa  kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29,2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 7

Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za marekani 375,418.
Katika kesi hiyo Malinzi wanakabiliwa na mashtaka 28 huku wenzake wakikabiliwa na makosa yasiyozidi manne.

Wakati kesi hiyo ikitajwa washtakiwa wote walikuwapo mahakamani na wanatetewa na wakili  Nehemia Nkoko, Dominician Rwegoshora na Abraham Senguji, Kashindye Thabiti.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search