Harbinder Sethi aieleza mahakama afya yake imeharibika.....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

MMILIKI wa IPTL, Harbinder Singh Sethi  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hali yake ya kiafya imezidi kuharibika .


Seth amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa


Harbinder Singh Sethi  wa kwanza kutoka kulia

"Hali yangu imeharibika sana naomba kupelekwa hospitali"alieleza Seth.
Baada ya kusema hayo Hakimu Shaidi aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili ili awe na afya njema waweze kuendelea na kesi.

"Huyu mtu anaumwa anaonekana hata kwa macho, suala la ugonjwa wake tuwaachie madaktari, hatuwezi kuendelea na kesi na mtu mgonjwa," alisema hakimu

Awali Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)Leonard Swai  alieza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haijakamilika na kwamba wamefanya mawasiliano kupata nyaraka kutoka nje.

Alidai  bado hawajachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili kwa sababu ya afya yake hivyo waliomba muda zaidi ili kukamilisha vipengele hivyo.Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Aprili 11,2018 kwa ajili ya kutajwa

Katika kesi hiyo, mbali na Sethi mshtakiwa mwingine ni James Rugemarila ambapo wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwemo kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya dola za kimarekan  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search