LHRC waijibu NEC....soma habari kamili na matukio360....#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
KITUO cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC) kimejibu hoja za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuatia kuhusika kutoa tamko lenye tuhuma za kupotosha baadhi ya mambo kupitia tamko la
umoja wa asasi za kiraia nchini (Azaki).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Naemy Sillayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni NEC kupitia
kwa mkurugenzi wa uchaguzi Kailima
Ramadhani ilikiandikia barua yenye Kumbukumbu. Na. Bi. 71/75/01/124 ya Februari
22, 2018 ikikituhumu moja kwa moja kuhusika katika upotoshwaji kwenye tamko la juu
ya taarifa ya hali ya usalama wa raia, haki za binadamu na utawala bora.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC
Naemy Sillayo amesema kituo hicho kirishiriki kama moja ya asasi zinazounda
umoja wa Azaki.
“Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu kama moja ya asasi zinazounda umoja wa Azaki hizo kimelezimika
kujibu hoja hizo kwani NEC katika tamko lake lililotolewa Ijumaa Februari 23,
2018 imekituhumu moja kwa moja LHRC kupitia kwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi, Bw.
Paul Mikongoti, kwa kutoa tamko lenye tuhuma za kupotosha baadhi ya mambo
kupitia tamko la hilo la umoja wa Azaki,” amesema Sillayo.
“Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu, kilishiriki kwenye tamko hilo kama mwanachama wa Azaki kwa
kutambua wazi kuwa lengo la tamko hilo ni kuimarisha hali ya haki za binadamu
na demokrasia nchini na si vinginevyo,” ameongeza.
Ameitoa wasiwasi NEC kuwa
hakukuwa na maslahi tofauti wala upotoshaji wa makusudi katika utoaji wa tamko
hilo.
Amesema kwamba kituo
kinakiri kufahamu kwa kina sheria na kanuni zinazoratibu chaguzi na kinatambua
kuwa lengo la Azaki haikuwa kubeza wala kuvunja kanuni hizo bali kutoa
mapendekezo kwa ajili ya mboresho ya chaguzi na hatimaye kuimarisha demokrasia
nchini.
Sillayo ameikumbusha
NEC kuwa tamko husika halikutolewa na LHRC bali lilitolewa na umoja wa Azaki
chini ya jukwaa la wakurugenzi wa Azaki hivyo haikuwa busara kuwashambulia wao moja
kwa moja.
No comments:
Post a Comment