MSD yaelezea upatikanaji dawa nchini....soma habari kamili na matukio360....#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

BOHARI ya Dawa nchini (MSD) imesema upatikanaji dawa muhimu zaidi (high priority list) ambazo ni 135 umefikia asilimia 90.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saal.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Banakunu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Dawa tunazo nyingi, hali ya upatikanaji wa dawa imeimarika, kwa mfano leo Machi 7, 2018 upatikanaji wa dawa muhimu zaidi (High priority list) ambazo ni jumla ya 135 umefikia asilimia 90 ukijumlisha na zile zilizopo kwenye maduka ya MSD,” amesema Bwanakunu.

Amesema dawa hizo zote zinahitajika katika vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya nchini.

Pia amesema upatikanaji wa dawa hizo muhimu zaidi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni kati ya asilimia 85 hadi 95, upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI na za kutibu malaria ni asilimia 100.

Wakati huo huo upatikanaji dawa za uzazi wa mpango ni asilimia 67 huku za kutibu kifua kikuu pamoja na ukoma ni asilimia 63.

Katika hatua nyingine MSD imesema imeanza kutoa huduma ya mifuko yenye vifaa vya kujifungulia kwa akina mama (Delivery Pack).

Bwanakunu  amesema  vifaa hivyo vitakuwa vikipatikana kwa bei nafuu na mfuko huo utakuwa na vifaa 12 na utauzwa kwa sh. 21,000.

Ametaja vifaa hivyo kuwa ni pamba kubwa (Cotton wool gm.500), mpira wa kuzuia uchafu (Macknitosh 1.5 mters), taulo ya kike ya wazazi (maternity pad) sindano ya kuzuia damu kupotea (Oxytocin injection) na mipira ya mikono (Surgical gloves 4 pairs).
Vingine ni nyembe za kupasulia (Surgical blade), kibana kitovu cha mtoto (Umbilical Cord clamp), dawa ya spirit, detol ya maji, dawa ya sindano ya ganzi (Lignocaine) mabomba ya sindano mawili na nyuzi za kushonea (Surgical Sutures).
Awali mkurugenzi huyo amesema MSD imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata ithibati ya kimataifa ya Ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2017-2020).


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

1 comment

  1. Jack Reacher Never Go Back is sequel to Tom Cruise movie named Jack Reacher. Second part is directed by Edward Zwick and producer are Tom Cruise,... USA delivery Soma

    ReplyDelete

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search