Tundu Lissu leo kufanyiwa upasuaji wa goti...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo Machi 14,2018 atafanyiwa upasuaji wa 19 katika goti lake kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.
Tundu Lissu
Upasuaji huo ni mwendelezo wa ambazo amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7,2017.
Taarifa ya Lissu aliyoitoa Machi 10,2018 akielezea afya yake alisema licha ya sasa kuweza kusimama bila msaada, amejuzwa na timu ya madaktari wanaomtibu kuwa kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo.
“Madaktari wangu wamesema wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo itachukua muda mrefu sana kuunga,” amesema.
Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) amesema madaktari wamemweleza hata mfupa huo ukiunga baada ya muda mrefu, hautaunga kwa namna utakaoondoa hatari ya kuvunjika baadaye.
“Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia Machi 14,2018, nitarudi Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, kwa ajili ya kufanyiwa operesheni hiyo,” alisema.
Alisema yuko katika mikono salama ya kitabibu chini ya madaktari Profesa Stefa Nijs na Profesa Willem-Jan Mertsemakers ambao amesema ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya.
“Hivyo, msiwe na hofu. Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza kupitia kwa madaktari bingwa hawa,” alisema.
Lissu aliema ataendelea kutoa taarifa za maendeleo ya afya yake kwa kadri itakavyohitajika akiwaomba Watanzania kumuunga mkono yeye na familia yake katika kipindi anachopitia.

No comments:
Post a Comment