Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane hatoshiriki katika mechi hadi mwezi Mei baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa alipata jeraha la kifundo cha mguu zaidi ya alivyodhaniwa hapo awali. (Mirror)
Harry Kane
Crystal Palace iko tayari kuuza haki zake za jina la uwanja wake wa Selhurst Park ili kuisaidia kujenga uwanja mpya utakaogharimu pauni milioni moja. (Evening Standard)
Everton wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Jack Wilshere kwa uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Mirror)
Liverpool ina hamu ya kutaka kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig mwenye umri wa miaka 22 Timo Werner. (Independent)
Huenda Manchester City wakashindwa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 25 Fred, ambaye anasakwa na Manchester United.(Times - subscription required)
Southampton wanatumai watamsajili mkufunzi Mark Hughes kuwa meneja wao mpya siku ya Jumatano. Mkufunzi huyo wa zamani wa Stoke amepewa kandarasi hadi mwisho wa msimu huu. . (Telegraph)
West Ham itamuajiri mkurugenzi wa soka mwisho wa msimu huu kwa lengo la kuimarisha mipango yake ya uhamisho , swala ambalo halijawafurahisha mashabiki wake. (Evening Standard)
Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis anamtaka mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama kocha mpya wa klabu hiyo. (Daily Star)
Mshambuliaji wa Middlesbrough mwenye umri wa miaka 26 na raia wa Denmark Martin Braithwaite anataka kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Bordeaux baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo msimu huu. (Evening Gazette, via Gold FM)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search