Serikali yabariki dawa za nguvu za kiume.... soma habari kamili na matukio360....#share


Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

SERIKALI imesajili dawa za asili tano ikiwamo ya nguvu za kiume na hadi kufikia Desemba 31, 2017  wametoa usajili kwa waganga 16,300 na vituo 212.

Pia waganga wote wa tiba mbadala walioweka mabango ya kutangaza magonjwa wanayotibu ikiwamo Ukimwi, kuyaondoa.

Dk Faustine Ndugulile

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk Faustine Ndugulile amezitaja dawa hizo  jijini Dar es Salaam kuwa ni Ujana, IH-Myoon, Coloidal Silva, Sudhi na Vatari.

Dk. Ndugulile ameagiza kukamatwa kwa waganga wote wanaotumia mashine za kupima magonjwa mbalimbali na kuondoa sumu mwilini kwani mashine hizo hazijasajiliwa popote na hawana vibali vya kufanya hivyo.

Dk. Ndungulile amesema matangazo hayo ni kinyume cha sheria ya Tiba asili na Tiba mbadala.

Amesema katika sheria hiyo mganga haruhusiwi kutangaza yeye ni nani, ana utaalamu gani katika kutibu, anapopatikana na mawasiliano lakini kwa sasa waganga hao wamekuwa wakiorodhesha magonjwa wanayotibu kitendo ambacho ni kinyume.

"Ni marufuku kujitangaza kwa vyovyote kwenye vipindi vya runinga, radio wala simu za mkononi,"amesema 

Ameongeza kuwa Baraza litaanzisha msako kwa wale wanaotoa matangazo na vyombo vya habari vitakavyotoa matangazo ya waganga ambao hawajasajiliwa navyo vitachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema msisitizo wao kwa mwaka 2018 katika Tiba asili na Tiba mbadala ni usajili wa mganga, kituo na dawa za asili.

Amesema wamesajili dawa chache kutokana na sheria hiyo kuanza kutumika mwaka jana, hivyo waganga wengi walikuwa bado hawajaifahamu.

Amefafanua kuwa sasa wameanza kupokea barua za maombi ya usajili wa dawa zao na kuwataka waganga hao kuacha kufanya ramli chonganishi ikiwa ni pamoja na kurudisha baadhi ya magonjwa na uchawi.

"Sheria ya usajili wa dawa imeanza mwaka jana kwa hiyo wengi walikuwa hajui, lakini hata hivyo mchakato wa kusajili dawa unahusisha idara nyingi, sasa hivi tuna maombi ya watu ambayo bado tunayafanyia kazi, niwatake tu ambao bado hawajapewa dawa zao kufanya hivyo kwasababu kuendelea kutoa huduma bila kusajili ni kinyume cha taratibu," amesema.

Msajili wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala, Ruth Suza amesema wamefanya Oparesheni Machi 6 na 7 mwaka huu, kuwasaka wale wanaotumia mashine za kupima na kuondoa sumu mwilini na watatangaza  idadi yao hivi karibuni. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search