Maalim Seif auzungumzia waraka wa maaskofu KKKT.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama
cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif ameunga mkono waraka uliotolewa mwishoni mwa juma
na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) na kutaka
wasihusishwe na masuala ya kisiasa.
Katibu Mkuu wa Chama cha CUF Maalim Seif, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipitakiwa kutoa maoni yake juu ya waraka
huo wakati wa maswali baada ya kuwasilisha mbele ya waandishi wa habari
maazimio ya kikao cha kamati ya utendaji ya chama cha CUF Taifa kilichofanyika Machi 25, 2018.
“Mimi kama mimi nimefarijika
ninaunga mkono kuona viongozi wa dini wanakemea mambo ambayo hayaendi vizuri na tusitafsiri kuwa wamejiingiza kwenye siasa,
kwa kuwa ni viongozi wa kiroho wanawajibu wa kuwatetea waumini wao, ningefarijika
sana kama na viongozi wangu wangefanya hivyo,” amesema Maalim.
Katika waraka huo
uliopewa jina la ‘Taifa Letu Amani Yetu’ na kusainiwa na Maaskofu 27 wa kanisa
hilo uliainisha changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa kwenye nyanja za
hali ya kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwemo suala la Katiba
Mpya.
Katibu Mkuu huyo
amesema kuwa lengo la Maaskofu hao siyo kuikosoa serikali bali ni katika hali
ya kutaka mambo yaende sawa ambapo ameeleza kufarijika kwa kuona taasisi
mbalimbali zikitoa matamko pale zinapoona mambo hayaendi kama inavyotakiwa.
Amewataka watanzani na
taasisi mbalimbali nchini kuendelea kupaza sauti na kuikumbusha serikali kuwa
jukumu lake la msingi ni kulinda usalama wa raia na mali zao.
Katika hatua nyingine Maalim Seif ametuma salamu za rambirambi kufuatia
vifo vya watu 26 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea juzi Mkuranga
Mkoani Pwani.
Ajali hiyo ilihusisha gari ndogo ya abiria aina ya
Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake
Kimanzichana – Mbagala Rangi tatu na gari nyingine aina ya Lori.
No comments:
Post a Comment