Maalim Seif: Lipumba mnafiki, mpotoshaji .....soma habari kamili na matukio360....#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif amedai Profesa Ibrahim Lipumba ni mpotoshaji, mnafiki na amekisaliti chama.


Pia Maalim Seif amekanusha kuwa yeye ndiye anayekidhoofisha chama na kwamba lengo la Profesa Lipumba si kujenga chama bali kukichafua.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Sief akizungumza katika kongamano la chama lililofanyika wilayani  Kinondoni kata ya Tandale jijini Dar es Salaam.

Juzi Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari alidai katibu mkuu huyo amekidhoofisha CUF kwa kutotekeleza azimio la baraza kuu la kufungua kesi mahakama kuu ya Zanzibar kupinga kufutwa matokeo ya uchaguzi wa wakilishi na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Pia alidai mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CUF ulianzishwa na Maalim Seif Sharif akiwa na lengo la kudhoofisha chama hicho na kuwakumbatia viongozi wa Chadema.

Maalim Seifa akizungumza jana katika kongamano la chama lililokuwa na lengo la kubadilishana mawazo juu ya hali, mwenendo na matatizo ya chama ili kuyatafutia ufumbuzi lililofanyika wilayani Kinondoni kata ya Tandale jijini Dar es Salaa, alisema madai hayo ni upotoshwaji.

“Anasema eti mgogoro uliopo ni mimi kung’ang’ania viongozi wa Chadema ni mnafiki mkubwa, aliyeunda Ukawa ni yeye mwenyewe, mtoto aliyemzaa mwenyewe anataka kumuua, Lipumba amekisaliti chama na asimtafute mtu wakumbebesha maiti,” amesema Maalim. Na kuongeza "lengo la Profesa Lipumba si kujenga chama bali kukichafua."

Akijibu kuhusu madai kutotekeleza maazimio ya baraza kuu ya kufungua kesi mahakama kuu Zanzibar kupinga kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi ili kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, amesema kuwa hakuna maazimio kama hayo.

Katibu mkuu huyo amesema lengo la CUF ni kuongoza serikali ni si kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwani hata akiwa katika serikali hiyo bado itaongozwa na ilani ya chama chenye rais.


Katika hatua nyingine Maalim ameendelea kusisitiza kuwa CUF ilishinda uchaguzi wa urais wa Oktoba 25, 2015 na kudai kuwa uchaguzi wa marudio ni haramu na serikali iliyopo ni haramu hivyo haitambui na hawezi kushirikiana nayo.

Amesema kwamba wataendelea kudai haki ya wazanzibar, na anaamini itapatikana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search