Manispaa ya Ilala kutumia bilioni 287 .....soma habari kamili na matukio369....#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
HALMASHAURI ya Manispaa
ya Ilala jijini Dar es Salaam, imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 kwa mwaka wa
fedha 2018/2019 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na matumizi ya
kawaida.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam likipitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizungumza na
waandishi wa habari kwa niamba ya Mkurugenzi baada ya kupitishwa kwa bajeti
hiyo, Mchumi wa Ilala Ando Mwanduga, amesema fedha hizo zimegawanyika katika
makundi mawili.
Ameeleza bajeti ya
mapato ya ndani yanayotokana na vyanzo vya halmashauri ni sh.bilioni 56.8 na
kwamba fedha inayobaki inatokana na ruzuku kutoka serikalini.
Amesema kama ilivyo
maelekezo ya serikali kwa mapato ya ndani wametenga asilimia 60 kwa ajili ya
miradi ya maendeleo na asilimia 40 kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
“Sasa ukikokotoa hapo
unapata kwamba kwenye miradi ya maendeleo ipo sh.bilioni 35 na bilioni kama 24
zipo kwa matumizi ya kawaida,” amesema.
Mwanduga amesema bajeti
hiyo imeongezeka kutoka sh.biloni 124 kwa bajeti iliyopita hadi sh.287 ya mwaka
huu wa fedha 2018/2019.
Awali akiwasilisha
mapendekezo ya mipango na bajeti Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za
Jamii Jacob Kissi amesema kamati yake inataraijia kutumia jumla y ash.bilioni
122.9.
“Sh.bilioni 95.3 kwa
ajili ya mishahara, sh.bilioni 8.1 kwa matumizi ya kawaida na bilioni 19.4 kwa
ajiliya miradi ya maendeleo,” amesema Kissi.
Ametaja miradi ya
maendeleo itakayotekelezwa kuwa ni katika elimu ya msingi,Idara ya elimu ya
sekondari, Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Idara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
Mingine ni Idara ya
Maendeleo ya Jamii ya Vijana na Idara ya Mifugo na Uvuvi.
No comments:
Post a Comment