UN waipongeza Tanzania....soma habari kamili na matukio360...#share
Na
Luteni Selemani Semunyu UNAMID
Umoja wa mataifa UN umeipongeza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Mkuu
wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao
za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.
Mwakilishi maalumu wa katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia
Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa
Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID
Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Hayo yalibainishwa na mwakilishi
Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Watoto
(Special Representative of Secretary general of Child Abuse and AA) Profesa
Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya
Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa
nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa
mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi
la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake katika kushughulikia
mambo ya msingi katika kudumisha Amani.
“Sina budi kuipongeza Serikali
chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi
Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika nzima katika
kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa
Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani” Alisema Profesa Virginia.
Aliongeza kuwa kutokana na
kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka na kuwataka
kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu
Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.
“ Najivunia Tanzania naweza
kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na Umahiri
wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika
kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.
Pia aliwataka Wananchi wa Sudan
kuiga Mfano wa Tanzania waliowasha mwenge katika kilele cha Mlima Kilimanjaro
kuwa ishara ya Amani Afrika na kumulika dhidi ya maovu mbali mbali
ikiwemo dhidi ya watoto kwa kuwasha moto wa amani utakaoangazia watoto
wote wa Sudan.
Aliongeza kuwa ni wajibu wa
Sudan kuuiga Tanzania kwa kuwasha moto wa Amani kwani wana kila sababu ya
kufanya hivyo bila kutegemea msaada wowote kwani ni nchi yenye rasilimali
nyingi za kiuchumi lakini kinachokwamisha ni Amani ili kujiletea maendeleo.
Mwakilishi huyo wa Umoja wa
mataifa mbali na kutembelea vijiji mbalimbali alitembelea kambi ya
Shangilitobaya inayokaliwa na Kikosi cha Tanzania chini ya kikosi cha 11
kinachoongozwa na Kanali William Sandy na kuwapongeza Askari wake kwa kazi
nzuri ya Ulinzi wa Amani Duniani kote.
Tanzania kupitia Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania linashiriki katika mpango wa Ulinzi wa Amani chini ya
Mwamvuli wa Umoja wa mataifa na Umoja wa Afika UNAMID nchini SUDAN ambayo sasa
inaingia hatua ya Pili ambayo majeshi ya Tanzania yameunganihswa katika kikosi
maalum ambacho kinaanza kazi katika safu za Milima ya jebel Marra Mashariki maeneo
ambayo hayakunufaika kwa kufikiwa na UNAMID kwa kipindi chote.
Wanajeshi wa Tanzania hivi
karibuni walipongezwa kuyafikia maeneo ya safu za Milima ya Jaber Mara
na kufanya Doria ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa UNAMID na
mashirika ya Umoja wa Mataifa kutokana na maeneo hayo kukaliwa na Waaasi na
ubovu wa Miundombinu.
No comments:
Post a Comment