Mbunge Mary Nagu ashikiliwa na polisi.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Hanang

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu anashikiliwa na jeshi la polisi akidaiwa kuichonganisha serikali na wananchi.


Dk Mary Nagu

Dk Nagu aliyewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa Serikali za awamu mbili zilizopita, anashikiliwa  na polisi kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara Msafiri.

Mkuu huyo wa wilaya ameiambia matukio360 kuwa hatua hiyo inafuatia mbunge huyo kuhamasisha wananchi wasichangie wala kujishughulisha na shughuli za maendeleo.

" Nimeagiza akamatwe kwa kuwa anawashawishi wananchi wasichangie wala kujishughulisha na shughuli za maendeleo, hivyo unapozuia jitihada za maendeleo maana  yake unaichonganisha serikali na wananchi," amesema

Pia amesema mbunge huyo amekuwa akihamasisha wananchi wasishiriki shughuli zinazofanywa na mkuu huyo wa wilaya.

Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo  ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya(CCM) amesema Nagu ataachiliwa mara baada ya taratibu kukamilika.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search