Saba wapandishwa kizimbani....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Watu saba akiwamo raia wa Zambia wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, wizi na utakatishaji wa fedha wa Sh milioni 120.5
Akiwasomea hati ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao,Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono jana kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Robert Silaa (26) ambaye ni wakala wa usafirishaji.
Isihaka Ngubi (25) dereva, Cathbeth Mlugu (35) Mlinzi wa Zambia Cargo and Logistic Ltd, Mrisho Mindu karani, Giften John (32), Maulid Said (40) karani, Kirby Ng'andu Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Zambia Cargo and Logistic Ltd.
Wakili Kombakono alidai kuwa kati ya Januari Mosi,2018 na Februari 6,2018 katika kampuni ya Zambia Cargo and Logistic Ltd iliyopo Dar es Salaam washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la wizi.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho cha Januari Mosi na Februari 6,2018 washtakiwa hao waliiba katoni 700 za korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya dola 54,180 sawa na Sh 120, 563,909.55 ambazo ni mali ya Barabara Trading Tanzania Limited.
Iliendea kudaiwa katika shtaka la utakatishaji fedha kuwa washtakiwa hao walijihusisha moja kwa moja na muamala wa katoni 700 za korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya Sh 120,563,909.55 wakati wakijua mali hiyo ilikuwa ni zao la wizi.
Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo yanayowakabili wote walikana na upande wa mashtaka alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Washtakiwa walipelekwa rumande kwa sababu shtaka la utakatishaji wa fedha kwa mujibu wa sheria halina dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Machi 9,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment