Meya Mwita ataka halmashauri kutoa ajira kwa watakaozika maiti... soma habari kamili na matukio360....#share


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MEYA wa  Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote  za jiji hilo  kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao  hawana  ndugu.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo  leo kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaeleza  madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji,kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.

Amefafanua hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.

“ Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba  jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao” amesema Mwita.

Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini hapo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza makubaliano hayo.

“Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema.

Amefafanua kuwa watu  wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa  hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali.

Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu wake katika kuzika marehu hao  kila halmashauri linajukumu la kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.

Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ya kuzika miili ya watu ambao wamefariki na hawana ndugu.

“Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka,” amesema Mwita.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search