Mfumuko wa bei wapanda...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2018 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.1 ikilinganishwa na asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Januari, 2018.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi (NBS) Ephraim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Hii inamanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo, amesema “Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula ingawa kuna bidhaa chache za vyakula zilizochangia,”.

Ametaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei kati ya Februari, 2017 na Februari, 2018 ni pamoja na mkaa kwa asilimia 17.6, gesi ya kupikia kwa asilimia 11.1, mafuta ya taa kwa asilimia 9.9.

Bidhaa nyingine ni petrol kwa asilimia 13.1, dizeli kwa asilimia 11.3, huduma za meno kwa asilimia 21.9, viatu kwa asilimia 3.4, mavazi ya wanaume kwa asilimia 3.4 na mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.8.

Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kwesigabo amesema nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.

Kwa upande wa Kenya amesema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 umepungua hadi asilimia 4.46 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search